Announcements

TANGAZO LA KUJIUNGA NA MAFUNZO KWA MWAKA WA MASOMO 2020/2021

Posted On: 23rd Jul, 2020

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

CHUO CHA VIWANDA VYA MISITU – MOSHI

NAFASI ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA TEKNOLOJIA YA VIWANDA VYA MISITU KWA MWAKA WA MASOMO 2020/2021

Mkuu wa Chuo cha Viwanda vya Misitu - Moshi anakaribisha maombi ya kujiunga na chuo kwa mwaka wa masomo 2020/2021.

A. Kozi zinazotolewa:

i. Astashahada ya Awali ya Teknolojia ya Viwanda vya Misitu (NTA – Level 4). Mafumzo ya mwaka mmoja (1);

ii. Astashahada ya Teknolojia ya Viwanda vya Misitu (NTA – Level 5). Mafunzo ya mwaka mmoja; (1);

iii. Stashahada ya Teknolojia ya Viwanda vya Misitu (NTA – Level 6). Mafunzo ya mwaka mmoja (1).

B. Sifa za mwombaji:

i. Astashahada ya awali ya teknolojia ya Viwanda vya Misitu;

 • Mwombaji awe na cheti cha kuhitimu elimu ya sekondari na ufaulu wa alama D katika masomo manne;
 • Masomo mawili kati ya hayo yawe aidha Biolojia au Kemia au Fizikia au Hesabu au Jiografia; na
 • Masomo mengine mawili yasiyo ya dini. Ufaulu wa somo la kiingereza utapewa kipaumbele katika uchaguzi.
 • ii. Astashahada ya Teknolojia ya Viwanda vya Misitu;

 • Mwombaji awe na cheti cha kuhitimu Astashahada ya awali ya Teknolojia ya Viwanda vya Misitu au Astashahada ya awali ya Ufugaji Nyuki au fani nyingine inayolandana na hizo kutoka chuo chochote kinachotambulika na Baraza la Elimu ya Ufundi (NACTE); AU
 • Mwombaji awe na cheti cha kuhitimu elimu ya kidato cha sita na awe amesoma michepuo ya sayansi na kufaulu katika masomo mawili kwa alama ya E na S.
 • iii. Stashahada ya Teknolojia ya Viwanda vya Misitu;

  Mwombaji awe na cheti cha kuhitimu Astashahada ya Teknolojia ya Viwanda vya Misitu au fani nyingine ya sayansi inayolandana na hiyo kutoka chuo chochote kinachotambulika na Baraza la Elimu ya Ufundi (NACTE).

  C. Jinsi ya Kutuma maombi:

  I. Mwombaji atatakiwa kujaza fomu ya maombi ya kujiunga na chuo, kusaini na kuituma fomu hiyo ikiwa na vielelezo vyote muhimu. Ada ya maombi ya kujiunga na chuo ni Shilingi za Kitanzania 10,000/= (elfu kumi tu) kwa Watanzania na Dola za Kimarekani 20.00 kwa wasio Watanzania;

  II. Fomu za maombi zinapatikana Chuo cha Viwanda vya Misitu, Moshi au kwenye tovuti ya chuo [www.fiti.ac.tz];

  III. Maombi yote yaambatanishwe na vivuli vya vyeti halisi na taarifa za matokeo. Endapo mwombaji atakuwa na Ufadhili, uthibitisho wa maandishi kuhusu Ufadhili huo utahitajika;

  IV. Mwombaji anatakiwa kulipa ada ya maombi kupitia control number;

  V. Ili kupata control number au kupata ufafanuzi wa jinsi ya kujiunga na chuo, mwombaji awasiliane na Afisa Udahili wa Chuo kwa namba: +255752 206 305 au +255717085141 au +255754 862 737.

  D. Tahadhari

  I. Kwa yeyote ambaye hatazingatia utaratibu uliotajwa hapo juu, maombi yake hayatafikiriwa. Aidha, mwombaji atakayewasilisha hati za kughushi atachukuliwa hatua za kisheria;

  II. Maombi yote yatumwe kupitia anwani ifuatayo:-

  Msajili wa wanafunzi,

  Chuo cha Viwanda vya Misitu,

  S. L. P. 1925,

  Moshi.

  Au kupitia barua bebe: info@fiti.ac.tz

  III. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 15 Septemba 2020.

  E. Taarifa kwa watakaochaguliwa;

  Majina ya watakaochaguliwa pamoja na maelezo ya kujiunga na chuo yatawekwa kwenye tovuti ya Chuo [www.fiti.ac.tz].