Entry Requirements

1. Astashahada ya awali ya Teknolojia ya Viwanda vya Misitu;

  • Mwombaji awe na cheti cha kuhitimu elimu ya sekondari na ufaulu wa alama D katika masomo manne. Masomo mawili kati ya hayo aliyofaulu yawe aidha Baiolojia au Kemia au Fizikia au Hesabu au Jiografia. Masomo mengine mawili kati ya hayo aliyofaulu yasiwe ya dini. Ufaulu wa somo la Kiingereza utakuwa kipaumbele cha ziada katika uchaguzi;

2. Astashahada ya Teknolojia ya Viwanda vya Misitu;

  • Mwombaji awe na cheti cha kuhitimu Astashahada ya awali ya Teknolojia ya Viwanda vya Misitu au Astashahada ya awali ya Misitu au Astashahada ya awali ya Ufugaji Nyuki au fani nyingine ya sayansi inayolandana na hizo kutoka chuo chochote kinavyotambulika na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Au Mwombaji awe na cheti cha kuhitimu elimu ya juu ya sekondari na awe amesoma michepuo ya sayansi na kufaulu katika masomo mawili kwa alama ya E na S;
3. Stashahada ya Teknolojia ya Viwanda vya Misitu;


  • Mwombaji awe na cheti cha kuhitimu Astashahada ya Teknolojia ya Viwanda vya Misitu au Astashahada ya Misitu au Astashahada ya Ufugaji Nyuki au fani nyingine ya sayansi inayolandana na hizo kutoka chuo chochote kinavyotambulika na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE);